Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark
Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark

Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark-Afisa wa Kisiasa

Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark; Ubalozi wa Denmark umekuwa ukishirikiana na Tanzania tangu mwaka 1963, ikifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kushirikiana na Denmark.

Katika kipindi cha miaka 60 iliyopita, Denmark kupitia Danida, imechangia zaidi ya TZS trilioni 50 katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, na kujenga mahusiano imara kati ya watu na taasisi.

Kwa kutambua nafasi ya Tanzania katika masuala ya kimataifa, Denmark imeamua kupanua ushirikiano wake na Tanzania.

Mbali na ushirikiano wa maendeleo, juhudi za kuimarisha biashara na uwekezaji, pamoja na majadiliano ya kisiasa kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa yanayoathiri nchi zote mbili, zinaendelea.

Kwa lengo la kufanikisha ushirikiano huu wa siku zijazo, Ubalozi wa Denmark unatafuta mtu mwenye ari na bidii, atakayechangia katika kuimarisha mtandao wa kisiasa wa ubalozi na kufanikisha malengo ya mazungumzo ya kisiasa ya manufaa kwa pande zote mbili.

Mahali: Dar es Salaam
Mwisho wa Kutuma Maombi: 17 Desemba 2024
Aina ya Ajira: Kazi ya Kudumu (Full-time).

Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark
Nafasi za Kazi kutoka Ubalozi wa Denmark

Majukumu Makuu ya Nafasi Hii

  • Kujenga mitandao thabiti ya ndani ya nchi na kuhakikisha kufikia wadau muhimu kulingana na vipaumbele vya ubalozi, ikiwa ni pamoja na masuala ya usalama wa kikanda.
  • Kuandaa uchambuzi wa maandishi na ripoti kuhusu usalama wa kikanda, pamoja na maendeleo ya kisiasa na kijamii yenye umuhimu kwa sera za kipaumbele za Denmark.
  • Kushiriki kikamilifu katika vikundi vya kazi na majukwaa ya uratibu yanayofaa.
  • Kusimamia ushirikiano mdogo na vituo vya tafiti (think tanks).
  • Kuendesha mazungumzo endelevu na watafiti wa Denmark na Tanzania pamoja na vituo vya tafiti.

Sifa na Vigezo

  • Kuwa na shauku kuhusu masuala ya kisiasa ya kimataifa, kikanda, na kitaifa.
  • Uwezo mzuri wa uchambuzi na kuandika kwa uwazi, ufupi, na umakini wa kitaaluma.
  • Sifa nyingine na maelezo ya kina yanapatikana katika tovuti ya Ubalozi wa Denmark:
    www.tanzania.um.dk

Usawa wa Fursa

Ubalozi unathamini usawa wa fursa kwa wote na unakaribisha maombi kutoka kwa watu wote wenye sifa bila kujali rangi, jinsia, dini, umri, au ulemavu.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yatumwe kupitia:
Barua pepe: recruitment@prospect-africa.net

Kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi hii, tembelea tovuti rasmi ya Ubalozi wa Denmark.

Makala nyinginezo: