Nafasi 7 za Kazi TANROADS
Nafasi 7 za Kazi TANROADS

Nafasi 7 za Kazi TANROADS – Novemba 2024

Nafasi 7 za Kazi TANROADS; Tanzania National Roads Agency (TANROADS) ni wakala wa serikali anayehusika na matengenezo na maendeleo ya mtandao wa barabara nchini Tanzania. TANROADS ina jukumu kubwa katika kukuza miundombinu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Wakala huu unasimamia mtandao mkubwa wa barabara kuu (trunk roads) na barabara za mikoa (regional roads), ukihakikisha usalama na ufanisi wa barabara hizo.

TANROADS ilianzishwa rasmi tarehe 1 Julai, 2000, kupitia tangazo la serikali lililochapishwa katika Gazeti la Serikali, Tangazo Na. 293 la 2000, chini ya kifungu cha 3(1) cha Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Lengo kuu lilikuwa ni kuboresha matengenezo na maendeleo ya barabara kwa kuzingatia ubora, ufanisi, na gharama nafuu.

Majukumu Makuu ya TANROADS

  • Kusimamia mtandao wa jumla wa barabara zenye urefu wa kilomita 35,000.
    • Kilomita 12,786 ni barabara kuu (trunk roads).
    • Kilomita 22,214 ni barabara za mikoa (regional roads).
  • Kuhakikisha barabara zote zinalingana na viwango vya Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 na marekebisho yaliyofanyika hadi mwaka 2015.
Nafasi 7 za Kazi TANROADS
Nafasi 7 za Kazi TANROADS

Nafasi za Ajira TANROADS – Novemba 2024

TANROADS imeweka wazi nafasi saba (7) za ajira kwa mwaka huu. Hizi ni fursa kwa wale walio na sifa zinazohitajika kushiriki katika maendeleo ya miundombinu ya barabara nchini.

Faida za Kufanya Kazi TANROADS

  1. Kuchangia maendeleo ya barabara na miundombinu ya Tanzania.
  2. Kuwa sehemu ya shirika linaloleta mabadiliko chanya kwa uchumi wa taifa.
  3. Fursa za kujifunza na kukuza taaluma yako katika sekta ya miundombinu.

Jinsi ya Kuomba Nafasi Hizi

  • Tafadhali soma maelezo ya kazi kwa undani kupitia kiungo kilichotolewa hapa:
    Soma Maelezo Kamili ya Nafasi za Kazi Hapa

TANROADS ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote. Tunawahimiza watu wa jinsia zote na wenye ulemavu kuomba nafasi hizi.

Makala nyinginezo: