Nafasi 14 za Ajira katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT); Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ni mojawapo ya taasisi za elimu ya juu nchini Tanzania, ikijulikana kwa kutoa mafunzo ya ufundi na uhandisi.
Taasisi hii ilianzishwa rasmi mwaka 1957 na imesajiliwa kikamilifu na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutoa programu za ufundi na uhandisi zinazotoa tuzo za Diploma ya Kawaida (Ordinary Diploma – OD) katika uhandisi, Shahada ya Uhandisi (Bachelor of Engineering – BEng), pamoja na Shahada ya Umahiri katika Uhandisi (Master of Engineering – MEng).
Historia ya DIT
Kwa kihistoria, DIT ilianzishwa mwaka 1997 kwa sheria ya bunge, “Sheria ya DIT Na. 6 ya mwaka 1997,” ili kuchukua nafasi ya Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam ambacho kilikuwa na historia ndefu ya kutoa mafunzo ya kiufundi nchini Tanzania. Historia hii inarejea hadi mwaka 1957, ambapo taasisi iliyoitangulia, Taasisi ya Ufundi ya Dar es Salaam, ilianzishwa kwa lengo kuu la kutoa mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Taasisi hii baadaye ilipanua wigo wake na kuanza kutoa mafunzo ya shule za sekondari za ufundi pamoja na mafunzo ya Wasidizi wa Ufundi kabla ya kuboreshwa mwaka 1962 kuwa Chuo cha Ufundi cha Dar es Salaam (DTC), taasisi ya kwanza ya mafunzo ya kiufundi nchini.
Nafasi za Ajira DIT – Oktoba 2024
Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam inatangaza nafasi 14 za ajira kwa mwaka huu wa 2024. Nafasi hizi zinajumuisha nafasi mbalimbali zinazohusiana na uhandisi, ufundi, pamoja na nyadhifa nyinginezo ndani ya taasisi.
Kwa wale wanaopenda kujitokeza na kukidhi sifa zinazohitajika, hii ni fursa ya kipekee ya kujiunga na taasisi inayoheshimika nchini na kutoa mchango katika kuendeleza sekta ya elimu ya ufundi na uhandisi.
Wahitimu wa programu za uhandisi, wataalamu wa ufundi, na watu wenye nia ya kujifunza zaidi wanahimizwa kuomba nafasi hizi za ajira. Kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi hizi, pamoja na vigezo na masharti ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya DIT au ofisi zao za utawala zilizopo Dar es Salaam.
Hii ni fursa nzuri kwa wale wanaotafuta ajira katika sekta ya teknolojia na uhandisi, ambapo utaweza kuwa sehemu ya taasisi inayotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiufundi nchini Tanzania.
APPLY AJIRA HIZO 14 KUPITIA LINK ZIFUATAZO
- POST: ARTISAN II (CIVIL ENGINEERING) MASONRY – 1 POST
- POST: ARTISAN II (ELECTRICAL ENGINEERING) – 1 POST
- POST: ARTISAN II (CIVIL ENGINEERING) – CARPENTRY – 1 POST
- POST: TECHNICIAN II (SOIL) – 1 POST
- POST: ARTISAN II (LEATHER TECHNOLOGY) – 1 POST
- POST: ARTISAN II (PLUMBING) – 1 POST
- POST: ARTISAN II (MECHANICAL ENGINEERING)-FITTER MECHANICS – 1 POST
- POST: TECHNICIAN II (ELECTRONICS AND TELECOMMUNICATION ENGINEERING) – 1 POST
- POST: TUTORIAL ASSISTANT – MECHANICAL ENGINEERING – 1 POST
- POST: TUTORIAL ASSISTANT – CIVIL ENGINEERING – 1 POST
- POST: TUTORIAL ASSISTANT – BIOMEDICAL ENGINEERING – 3 POST
- POST: ASSISTANT LECTURER – (OIL AND GAS ENGINEERING) – 1 POST
Makala nyinginezo:
Leave a Reply